Kongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Alli amewataka watumishi wa idara ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kuendelea kuwajibika na kuwahudumia wananchi bila ubaguzi wala chuki.
Ameyasema hayo leo wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea mradi wa Duka la Dawa katika hospitali ya Wilaya ya Hai ili kujionea huduma zinazoendelea kutolewa kwenye duka hilo tangu lilipozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2018.
“Madaktari wetu tunawapenda sana naa tunajua mnafanya kazi ngumu masaa 24 jambo moja napenda kuwashauri ni kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa itakayowapa faraja”
“Pia tunao wazee wetu; tuwape kipaumbele kwenye kupata huduma kwani wao wametulea hadi kufikia hapa tulipo na ndio waasisi wa Taifa letu” Amesema Mkongea Ali.
Amewataka watumishi hao wa afya kutekeleza wajibu na majukumu yao ya kuwahudumia wagonjwa kwa moyo wao wote kwani ndiyo kazi waliyotumwa na serikali kuhudumia watu wake hasa wananchi wa kawaida.
Sambamba na hili amewataka watumishi wote wa umma kwenye kada mbalimbali kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na uadilifu na kukemea tabia ya baadhi ya watumishi kuchukua mali na vifaa vilivyonunuliwa na serikali kwa ajili ya matumizi ya umma na kuvitumia kwa matumizi binafsi.
Aidha amewataka wananchi kutumia kwa vizuri huduma wanazopatiwa na serikali ikiwemo vyandarua vinavyogawiwa kwa wajawazito ili kuwakinga na ugonjwa wa malaria na kuachana na tabia ya kutumia vyandarua kwa matumizi yasio sahihi kama kufunika buastani za mboga au kuvulia samaki.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 umetembelea Duka la Dawa katika hospitali ya Wilaya ya Hai lililojengwa kwa shilingi 41,485,900 ambalo lilizinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 ambalo linatoa huduma saa 24 na kuridhishwa na utendaji wa duka hilo kuanzia ujenzi wake, mifumo ya kuagiza dawa pamoja huduma zinazotolewa kwa wagonjwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai