Mkuu wa wilaya ya Hai mshikizi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Moshi Said Mtanda amewataka waalimu na watumishi wa umma kwa ujumla kujitokeza kupata chanjo ya Uvico-19 lengo likiwa ni kujikinga na virusi vya ugonjwa huo.
Mtanda ameyasema hayo wakati akifungua semina ya chama cha walimu UWT wilaya ya Hai katika ukumbi wa Hai Club na kutoa rai kwa wawakilishi wa walimu kuwa mstari wa mbele katika zoezi la kuchanja ikiwa ni pamoja na kuwahasisha wengine katika zoezi hilo.
“Wito wangu kwa walimu wote na nyie wawakilishi wa walimu kwenye shule zenu, kwanza sisi wenyewe tuchanje baada ya hapo tuwaambie wengine wachanje, hii ni hiyari yenye lazima ndani yake lakini pia biblia inasema tuzitii mamlaka na waislamu wanasema mtii Mwenyezimungu mtii mtume Muhammad na wale wote wenye mamlaka miongoni mwenu”
“Sasa mamlaka ikisema jamani chanjeni alafu wewe mtumishi wa umma ulioko chini ya mamlaka hiyo hujachanja maana yake wewe siyo mtiifu kwa mamlaka”
Aidha baada ya chanjo ya Uvico-19 kuingia hapa nchi Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan aliongoza zoezi la chanjo hiyo kwa yeye mwenyewe kuchanjwa ikiwa ni ishara ya kwamba chanjo hiyo ni salama kwa watanzania wote.
Naye katibu tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wella wakati akimkaribisha mkuu wa wilaya akawataka watumishi wa umma kila mmoja kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa ufanisi
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai