Watumishi wa umma kote nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia sheria zote za Serikali ambazo hupangiwa na mwajiri.
Katibu wa Kamati ya ushauri ya wanawake TALGWU taifa Christina Kiwi ametoa rai hiyo alipozungumza na wafanyakazi Wanawake ambao ni wanachama wa TALGWU wilaya ya Hai kwenye ukumbi wa hospitali ya wilaya hiyo lengo likiwa ni kuwakumbusha wajibu na haki za msingi mahali pa kazi.
"Sisi viongozi wa vyama tunasimama kati ya mwajiriwa na mwajiri ikiwa ni pamoja na kusisitiza watumishi wa umma tufanye kazi kwa bidii, tufanye kazi kwa kwa kufuata sheria zote za Serikali ambazo unapangiwa na mwajiri"
"Mwajiri pia anatakiwa atekeleze zile haki zake zote za msingi ambazo mwajiriwa anapaawa kuzipata"
Kwa upande wake mratibu wa masuala ya kijinsia TALGWU taifa Christina Mang'ana akizungumza kwenye kikao hicho ameeleza kuwa vyama vya wafanyakazi vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu kwa lengo la kuwasaidia wafanyakazi endapo watakutana madhila mbalimbali kazini.
TALGWU ni chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa ambacho kina jukumu la kuelimisha, kutetea na kulinda ajira na ujira wa wanachama wake kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na nyaraka mbalimbali za kazi
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai