Serikali imewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na ubunifu huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa na wananchii wake.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Hatibu Kazungu mapema leo Disemba 11 wakati wa kikao na watumishi wa Wilaya ya Hai alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kujadili namna bora ya kutekeleza kazi za serikali katika wilaya hiyo.
Amewakumbusha viongozi na watumishi kuwa changamoto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu ikiwemo maisha ya utumishi hivyo ni vizuri watumishi na viongozi kupata muda wa kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amemweleza Katibu Tawala huyo kuwa halmashauri inafanya oparesheni maalumu ya kukusanya mapato ya serikali yanayotakiwa kulipwa na wananchi kwa mujibu wa sheria.
Sintoo amewashukuru watumishi wa halmashauri kwa ushirikiano wanaouonesha katika utekelezaji wa kazi na majukumu wanayopatiwa bila kujali changamoto wanazokutana nazo huku akiwaahidi kuendelea kupunguza changamoto kadri hali itakavyoruhusu.
Hata ivyo Katibu Tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wella ameeleza kuwa wao kama wasiamamizi wakuu kwenye wilaya kwa kushirikiana na watendaji wa serikali za mitaa watahakikisha wanayatendea kazi maelekezo yote waliyopewa ili kutatua kero za watumishi na kufanya kazi zao wakiwa na amani na kutimiza malengo waliojiwekea.
Pia ametoa shurkani kwa ugeni huo wa Katibu Tawala wa mkoa kwani ni vyema kwa viongozi wa juu wa kiserikali kuwatembelea watumishi na kuzisikiliza kero zao na kuzitatua ili kuongeza hari kubwa ya ufanyaji wa kazi kwa faida ya Taifa na jamii kwa ujumla.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai