Wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao kipindi cha likizo na nyakati nyingine katika kuhakikisha wanakuwa na maadili mazuri ili kupunguza matukio ya unyanyasaji na ukatili kwa watoto
Hayo yamebainishwa na Saumu Daffa afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Hai, ambapo amesema hapo awali wawakilishi kutoka ustawi wa jamii pamoja na polisi walikuwa wakitoa elimu endelevu kuhusiana na ukatili wa jinsia kwa watoto
Aidha amesema wazazi wengi wameshindwa kufanya jukumu la malezi kwa kutokuwa karibu na watoto, wengi wao wakikimbizana na jukumu la kutafuta pesa jambo ambalo linawapa wakati mgumu walimu kuwa karibu na watoto kama wazazi
Ameongeza kuwa maeneo ya kata ya Masama Rundugai kumekuwa na wimbi kubwa la watoto kutoka jamii ya wafugaji, wengi wao wakiwa sokoni wakiuza bidhaa mbalimbali wakati wa likizo na kwenda kwenye vijiwe vya kuonesha Tv jambo linanohatarisha usalama wao
Hata hivyo amesema elimu iliyotolewa imeleta mafanikio makubwa kutokana na kupungua kwa idadi ya watoto wanaoenda sokoni muda wa masomo na huku wengine wakiendelea kupewa elimu zaidi ili kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai