Katika kuhakikisha watoto katika jamii ya Kitanzania wanapatiwa haki zao za kimsingi ikiwemo elimu na malezi bora Wazazi wametakiwa kutambua wajibu wao ikiwa ni pamoja na kutenga muda wakukaa na kuangalia maendeleo ya watoto wao kwa wakati wote.
Rai hiyo imetolewa hii leo June 16 2019 na Katibu tawala wilaya ya Hai Bi. Upendo wella wakati akizungumza katika maazimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika ambapo kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Kijiji cha machame Nkuu kata ya machame Mashariki wilayani Hai.
Amesema kuwa jamii ya sasa hasa wazazi kwakiasi kikubwa wamejikita kwenye shughuli zao za kila siku hali inayosababisha kusahau wajibu wao kwa watoto na kusababisha kukosa haki ya kutunzwa na wazazi wao.
"Hatuna budi kuangalia upyaa mtizamo wetu kwa watoto kama wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhusu majukumu yetu kwa watoto kwa malezi na makuzi kwa watoto,kina mama wengi Kilimanjaro tumejikita zaidi kwanye kufanya shughuli/za maendeleo, lakini pia tunatakiwa tutenge muda kwaajili yakuangalia maendeleo ya watoto wetu na kufuatilia mienendo ya watoto wetu natusjikite tu kwenye shuguli za maendeleo peke yake" Amesema Pendo wella.
Aidha amesema jukumu lakulea na kutunzwa ni wajibu wa wazazi na jamii yote hivyo kila mmoja anawajibu wakuhakikisha watoto wanakuwa na kutunzwa katika mazingira salama na kwamba wajibu wakwanza upo mikononi mwa wazazi.
"Kina mama tunawahasa wawape watoto haki yakuzaliwa, kuna kunyimwa haki ya kuzaliwa kwa kutoa mimba, na jua wapo wenzetu ambao wanaamini kwamba ni haki ya mama kuzaa au kutokuzaa,nashauri kuchagua kutokupata ujauzito na hatimae kutoa na kumkosesha mtoto haki ya kuishi" Ameongeza.
Ameongeza kuwa kutokana na tatizo la mimba za utotoni kumechangia watoto hao kukosa haki ya kupata elimu nakwamba swala hilo pia limeonekana kuwa changamoto katika wilaya ya Hai hasa katika shule za sekondary, hivyo ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa pamoja katika kumlinda mtoto ikiwa ni pamoja na kuwafichua wanaofanya vitendo hivyo.
"Suala la ujauzito limekuwa likiongezeka hususa nikatika shule za sekondary, pia utandawazi umechangia sana kwahiyo wazazi na jamii tutoe ushirikiano katika kuwafichua wanao wapa mimba kuliko kumalizana kinyumbani kwasababu anaeathirika ni mtoto na maisha yake yanapotea moja kwa moja, nitoe wito kwa wana Hai nakilimnjaro kwa pamoja katika kuhakikisha tunawalinda watoto wetu ili wasiweze kupata uajauzito" Amesisitiza.
Pia amewaasa wanafunzi kuepukana na vishawishi wanavyo kumbana navyo kwani vitasababisha kukatisha kukatisha masoma nakutokufikia malengo ya baadae.
Maadhimisho hayo mwaka huu yameambatana na kauli mbiu isemayo "Mtoto ni msingi wa taifa endelevu, tumtunze, tumlinde na kumuendeleza".
Tarehe 16 Juni ya kila mwaka ni siku ya 'Mtoto wa Afrika', siku maalum ambayo inakumbukwa kutokana na jinsi ambavyo watoto wa shule wa Kiafrika waliuawa kikatili na makaburu eneo la Soweto nchini Afrika Kusini wakipinga unyanyasaji uliokuwa ukiendelea.
Tukio hilo lilitokea mnamo Juni 16, 1976, ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya waandamanaji 20,000 walihusika, huku makadirio yakiwa ni zaidi ya wanafunzi 176 hadi 700 inatajwa kuwa walipoteza maisha.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai