Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Kassim Majaliwa amepiga marufuku uchangishwaji wa michango isiyokuwa ya lazima bila ya kuwepo kwa kiali cha Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri.
Akizungumza wakati akihutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Hai katika viwanja vya Bomani Mjini Bomang’ombe Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa pale ambapo wananchi wataona inafaa kuchangia miradi ya maendeleo katika maendeleo ya shule lazima wapate kibali cha Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Katika suala la umeme Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. John Magufuli anataka kuona kuwa kila nyumba ya mtu inakuwa na umeme unaowaka na kutoa punguzo katika gharama za ufungaji kutoka shilingi laki tatu na elfu themanini hadi kufikia shilingi elfu ishirini na saba kwa wanananchi waishio maeneo ya vijijini.
Aidha pia katika sula la maji amesema kuwa upo mpango wa kujenga bomba la maji kutoka wilayani Rombo kupitia wilaya ya Siha hadi wilaya ya Hai ambapo maji hayo yatatumika wilayani Hai.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema bado dirisha la usajili wa wanafunzi lipo wazi huku akitoa rai ya kulindwa kwa watoto wa kike kuhakikisha wanasoma na kuhitimu masomo na kumaliza elimu yao ili kutimiza ndoto zao.
Naye mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira amesema kuwa mkoa uko tayari kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na serikali ikiwemo kuimarisha uchumi wa wafugaji kwa kuwajengea wafugaji ranchi za mifugo ili kupata thamani ya mazao yao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai