Wilaya ya Hai imeadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya usafi katika soko kuu la walaji Bomang’ombe pamoja na hospitali ya wilaya hiyo kwa kufyeka nyasi kuzunguka eneo hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amesema kutokana na taka zinazozalishwa katika maeneo ya soko na hospitali wameona ni vyema kupitia siku ya muungano kwa kufanya usafi maeneo hayo ikiwa ni jitihada za kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa na mazingira masafi.
Ameongeza kuwa usafi ni jukumu la kila mmoja huku akiwataka wananchi kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuwa na utaratibu wa kufanya usafi kila wakati kwenye maeneo yao ya makazi na biashara.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Hai Zephania Gunda amesema kuwa wameendelea kusimamia shughuli za usafi wa mazingira kwa mujibu wa sheria ya mamlaka ya mji mdogo ya mwaka 2016 iliyorekebishwa mwaka 2020 ikiwa inamtaka kila mtu katika eneo lake awe na chombo cha kuhifadhia taka na kwenda kuzitupa eneo husika lililotengwa rasmi.
Aidha walioshiriki katika zoezi hilo la usafi ni pamoja na mkuu wa wilaya ya Juma Irando, mkurugenzi mtendaji, kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Hai,viongozi wengine pamoja na wananchi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai