Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imelenga kuunda chama maalumu cha akiba na mikopo (Saccos) ya wanawake itakayowawezesha Kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya Jamii Wilaya ya Hai, Lukas Msele alipokutana na kufanya kikao na viongozi wa Vikundi vya Wanawake wilayani Hai wapatao 239, huku lengo kubwa likiwa nikuhamasisha juu ya Uundwaji wa SACCOS Ambayo itawahudumia wanawake wote wa wilaya ya Hai.
Amesema kuwa SACCOS hiyo itakuwa suluhisho kubwa na pia itawawezesha kina mama hao kupata mikopo mikubwa pindi watakapo hitaji kulingana na akiba zake atakazo kuwa ameziweka, tofauti na mikopo midogo ambayo hivi sasa wanaipata kwenye vikundi.
"Akina mama wamekuwa na mahitaji mengi na wamekuwa ni uti wa mgongi katika kuakikisha maendeleo ya jamii hasa katika familia, kwa hiyo tumeona ni muhimu kuweza kupanua wigo wakujipatia rasilimali, kweli wamekiri wazi kwamba vikundi vimekuwa msaada mkubwa kwao, na sasa tukaona tuunde saccos ambayo itakuwa ni suluhisho kubwa pindi mtu anapohitaji mkopo mkubwa " Amesema Msele.
Aidha ameongeza kuwa hadi hivi sasa tayari wameshaunda uongozi wa mpito utakaosaidia kushughulikia hatua za awali zakuunda saccos hiyo na kusema kuwa hadi ifikapo mwaka wa fedha wa serikali 2019/2020 inategemewa kukamilika baada ya kupata usajili kutoka kwa mrajisi mkuu wa serikali.
Kwa upande wao baadhi ya akina mama walioudhuria kikao hicho Bi. Janeth Maiko na Bi. Halima Abdala, wamesema kuwa wamefurahishwa na wazo hilo la kuanzishwa kwa soccos hiyo na kuwa itawafanya waondokane na umaskini, huku wakiwasihi kina mama wengine kujitokeza na kujiunga na sacoss hiyo pindi itakapoanzishwa.
Aidha wamesema kuwa itawasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo sehemu sahihi yakupata mkopo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai