Zaidi ya wanachi 27,000 wa kata za Weruweru, Mnadani na Masama Rundugai wanatarajia kunufaika na huduma ya afya kutoka katika kituo cha afya kinachojengwa katika kijiji cha Longoi kata ya Weruweru kinachokadiriwa kugharimu zaidi ya milioni 500 kutoka katika mapato ya ndani.
Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho uliofanyika leo katika Kijiji cha Longoi Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amesema ujenzi wa kituo hicho ni maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kwenda kwa wasaidizi wake lengo likiwa ni kuwaondolea kero wananchi maeno ambao hawana huduma hiyo tangu nchi ipate uhuru.
Amesema fedha za awali za ujenzi wa kituo hicho kiasi cha shilingi 388,552,415, kimetokana na michango ya vyama vya ushirika wilayani humu na kwamba kukamilika kwa ujenzi huu utakipa heshima ushirika ambao kwa mingi mingi sasa umekuwa ukituhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha.
“milioni 388 itamaliza jengo la maabara ya upimaji, jengo la wagonjwa wa nje na jengo la mama na mtoto ,na akina mama waliokuwa wanatoka hapa wanavuka kale kadaraja kareli usiku wa manane wanapitia shirimgungani hadi mijongweni hadi shirimatunda hawatakwenda tena huduma zenu sasa zimeletwa hapa”alisema Sabaya.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa Kituo hicho Mganga mkuu wa wilaya Dr.Irene Haule amesema wazo la ujenzi wa kituo hicho cha Afya lilitolewa na mkuu huyo wa wilaya kwakushirikiana na kamati ya ulinzi na Usalama na kwamba kitawasadia wananchi wa kata hizo ambao baadhi yao wamekuwa wakitembea umbali zaidi ya km 20 kufuata huduma za Afya katika katika hospitali ya Wilaya.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo ameahidi kuzisimamia kikamilifu fedha hizo na kuhakikisha kuwa ujenzi wa kituo hicho unakamilika kwa wakati huku akiwataka wananchi wa eneo hilo kutoiba wala kuaribu mioundo mbinu ya mradi huo na kwamba yeyote atakaebainika atachukuliwa hatua kisheria.
Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Longoi; Mwajuma Athumani na Miraji Athumani wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuwapelekea kituo hicho cha afya kwani wamekuwa wakitumia gharama kubwa kufuata huduma za afya na wakati mwingine wamekuwa wakipoteza ndugu zao kutokana na huduma hizo kuwa mbali.
Wilaya ya Hai ina jumla ya vituo vya kutolea huduma 60 ambavyo kati ya hivyo vituo 2 Ni hospitali ya wilaya na hospitali teule ya Machame ambapo kati ya hivyo vimo vituo vya binafsi na vya mashirika ya dini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai