“Katika kipindi hiki cha ugonjwa; watu wetu wasitindikiwe na kitu kwa kudhulumiwa kwa sababu ya ugonjwa huu. Tulikuwa tunanunua sanitizer shilingi 2,500; leo hii watu wameuza shilingi 10,000 hadi 15,000”
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amemwaagiza afisa biashara katika wilaya hiyo kuwakamata wafanyabiashara na kuyafunga maduka yote ambayo yatabainika kupandisha bei ya bidhaa zinazotumika kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona ikiwemo barakoa na vitakasa (sanitaizer).
“Tukikuta uthibitisho wa namna yoyote kuwa umetumia nafasi hii ya watu wanaooteseka wakati ambapo Taifa linajitahidi khakikisha usalama wa kila mtu; ukapandisha bei; tutalifunga duka lako.
Ameagiza kuanza mara moja kwa ukaguzi wa dharura katika maduka yanayouza vifaa hivyo ili kuhakikisha kuwa vinawafikia wananchi kwa bei inayotakiwa ili waweze kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid 19).
Ole Sabaya ametoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi wa dini kabla ya kuanza kwa ibada maalum ya kumuomba Mwenyenzi Mungu aliepushe Taifa na ugonjwa wa Corona ambao sasa ni janga la dunia.
Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa wamejipanga kusambaza sanitaizer kwenye baa na hoteli zote wilayani humo bure ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi na kujikinga na ugonjwa huo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewataka viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuwaelimisha waumini wao kuhusu ugonjwa huo ili kuwasaidia kuepuka taarifa za uongo zinazosambaa na kusababisha taharuki na hofu kwa jamii kuhu akikumbusha kuwa hofu inaweza kusababisha madhara makubwa iwapo itaachwa itawale wanannchi.
Sintoo amewataka viongozi wa dini kusimama na kuitetea nchi na kufanya maombi juu ya janga hilo linaloikabili dunia kwa sasa.
Akizungumza kwa niaba ya viongo wengine, Hussein Mwanja amesema kutokana na hali ilivyo kwa sasa waumini wa dini zote wanatakiwa kujiwekea utaratibu wa kusali nyumbani ili kuondokana na msongamo kama serikali inavyoelekeza
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai