Rai imetolewa kwa wananchi wa wilaya ya Hai kuhakikisha kuwa wanapanda miti katika maeneo ya nyumba wanazoishi ili kutunza mazingira.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo katika zoezi la ugawaji wa miche ya miti elfu tano kwa wananchi wa Mji Mdogo wa Bomang’ombe.
Sintoo amegawa miche hiyo kwa wenyeviti wa vitongoji kumi na saba na wakuu wa shule kwenye hafla iliyofanyika katika ofisi za halmashauri hiyo kwa lengo la kuimarisha utunzaji wa mazingira ya wilaya.
Pia Sintoo amewaagiza watendaji wa Kata na vijiji pamoja na Mkuu wa idara ya maliasili kuhakikisha wanasimamia zoezi la kupanda na kutunza miti kwenye vitongoji vyote kumi na saba ili kufanikisha azma ya kufanya Wilaya ya Hai kuwa ya kijani.
Kwa upande wake Mtendaji wa Mamalaka ya Mji Mdogo Noel Nkoo amesema kuwa zoezi hilo la upandaji miti linatarajia kuchukua muda wa mwaka mmoja kwa kupanda miti laki moja na kwa awamu ya kwanza ikiwa ni miti elfu kumi kugwanywa katika shule 21 na vitongoji kumi na saba.
Hata hivyo Nkoo amewataka wananchi kukataa kuuziwa miti hiyo kwani inatolewa bure na Halmashauri ili kutunza mazingira ya wilaya ya Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai