Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Elia Machange amewataka watumishi wa halmashauri hiyo watakaoshiriki zoezi la kusajili vizazi hai kwa watoto chini ya miaka mitano kufanya kazi hiyo kwa weledi huku wakiwahudumia wananchi wote wenye kuhitaji huduma hiyo.
Akizungumza mapema leo 29/07/2020 kwenye ukumbi wa halmashauri wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa watumishi wa halmashauri hiyo watakaoshiriki zoezi la kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto.
Machange amewataka watumishi hao kutumia taaluma na nafasi zo kwenye jamii kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa zoezi la kusajili watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano waliopo kwenye jamii wanafikiwa.
Aidha Machange amewataadharisha washiriki wa mafunzo hayo kuwa wanatakiwa kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa na kuhakikisha kuwa watoto waliozidi umri unaotakiwa wa miaka mitano hawahusishwi na zoezi hilo bali wazazi wao washauriwe kufuata taratibu zinazowafaa watoto hao.
Naye Mratibu wa Huduma za afya ya Uzazi na Mtoto wilaya ya Hai Verdiana Michael amesema mafunzo kama haya yatafanyika kwenye ngazi ya kijiji ili kutoa nafasi kwa wananchi wote kupata uelewa na kufahamu umuhimu wa zoezi hili.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai