Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imekabidhi zaidi ya shilingi milioni thelathini na moja kwa vikundi vya wajasiriamali ikiwa ni kutekeleza mipango ya serikali kuwainua wananchi wake kiuchumi na kuleta maendeleo kwenye jamii.
Akikabidhi hundi ya fedha hizo Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya amemtaka Afisa Maendeleo wa wilaya kufanya tathmini ya matumizi ya fedha kwenye vikundi vilivyokwisha patiwa mikopo hiyo pamoja na kuwapa ushauri wa namna ya kuimarisha biashara zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amesema kuwa halmashauri yake itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kutokana na 10% ya makusanyo ya mapato ya ndani ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali.
Mmoja kati ya mwanakikundi cha Ebeneza kilichopo machame kinachojihusisha na kilimo cha mbogamboga Naomi Changari ameishukuru serikali kwa kuanzisha utaratibu wa utoaji wa mikopo na kusema kuwa fedha hizo zimekuwa chachu ya maendeleo kwa wajasiriamali katika wilaya hiyo.
Naye katibu wa kikundi cha TAUWA kilichopo Kambi ya raha Shabani Omary amesema kuwa wamefurahi kupata kile walichokua wanakisubiri na wameishukuru serikali kwa kutambua changamoto za vijana na kilichobaki ni kwenda kufanyia kazi kile walichopata na kuhakikisha kurejesha ili kuwezesha vikundi vingine kukopeshwa.
Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri ya wilaya Hai imefanikiwa kutoa mkopo wa shilingi 179,602,904 kwa vikundi vya wajasiriamali vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kufanikisha miradi mbalimbali ya kujiongezea kipato.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai