Ushirikiano kati ya viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro umepelekea kushika nafasi ya kumi kitaifa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani katika halmashauri.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Taifa Heri James wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM, wilaya ya Hai pamoja na watumishi mara baada ua kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho.
Kheri amesema kuwa juhudi zilizoonyeshwa na waatalamu wa halmashauri hiyo katika ukusanyaji wa mapato ya ndani imepelekea kupata mafanikio katika ukusanyaji pamoja na kuondoa manunguniko ya utoaji wa huduma kwenye jamii.
Aidha, Mwenyekiti huyo amepongeza juhudi zinazooneshwa na mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya katika kusimamia utekezaji wa ilani ya CCM, na kujali maslahi ya wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani, mkuuwa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema kuwa halmashauri hiyo Imefanikiwa kuongeza mapato ya ndani katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka 2018/2019.
Ole Sabaya amesema halmashauri kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama imefanikiwa kuongeza mapato katika soko la matunda na mbogamboga la sadala kutoka shilingi laki sita hadi shilingi milioni 2 kwa siku za soko huku ushuru wa mabasi standi ya Bomangombe ukiongezeka kutoka laki mbili hadi shilingi laki nne kwa siku.
Mkutano wa halmashauri kuu maalumu ya CCM wilaya ya Hai imefanyika katika viwanja vya Panone wilayani Hai kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika wilaya ya Hai kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi Disemba 2018 ambayo imeonesha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika sekta za afya, elimu, maji, usafiri, umeme na sekta nyingine zilizofanikiwa kutokana na mwongozo mzuri uliowekwa kwenye ilani hiyo pamoja na usimamizi madhubuti wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt, John Pombe Magufuli.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai