Katika wiki ya upandaji miti mwaka 2020 Halmashauri ya wilaya ya Hai kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili kwa kushirikiana wananchi wa Kitongoji cha Maiputa wamefanya zoezi la kupanda zaidi ya miti 3000 katika tindiga la Boloti ili kuimarisha utunzaji wa mazingira kwa maeneo ya hifadhi za serekali.
Akizungumzia zoezi hilo Afisa Maliasili wilaya ya Hai Mbayani Molell amesema kuwa katika wiki ya upandaji miti wilaya ya Hai imeweka mkakati wa muda mrefu wa kupanda miti katika chanzo hicho cha maji kwa ajili ya kukitunza na kukiendeleza kwani kimekuwa msaada mkubwa kwa wakulima wanaotumia maji yake kwenye umwagiliaji.
Molell amesema kuwa pamoja na kupanda miti hiyo wanawapa wananchi elimu ya utunzaji wa mazingira ili kuhahakisha kuwa miti iliyopandwa inalindwa na kutunzwa ipasavyo huku akibainisha wazi kuwa endepo akibainika mtu yeyote anayeharibu mazingira atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Maiputa Benson Ndosi amesema kuwa wameamua kujitolea kupanda miti eneo hilo na kwamba wako tayari kulinda na kutunza miti hiyo na wapo watu maalum kwa ajili ya kuitunza.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kikundi cha Isarie foresta cha utunzaji wa mazingira Ngarami Swai amewataka wananchi wa eneo hilo kushirikiana kwa pamoja katika kulinda na kuitunza miti hiyo na sio kuachia viongozi peke yao kwani miti ni faida kwa watu wote.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai