Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imepokea fedha kiasi cha Shilingi 949,100,000.00 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa ya awali na msingi katika shule saba za msingi za Wilaya hiyo.
Taarifa imetolewa na Afisa elimu msingi Wilayani hapo Huseni Kitingi katika Kata za Machame Narumu na Masama Kusini alipokuwa akiutambulisha mradi mpya wa BOOST unaotekelezwa katika Wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa Kitingi amesema Shule ya msingi msamadi na shule ya Msingi Narumu ni Miongoni mwa shule saba za wilaya hiyo zilizopatiwa fedha kwaajili ya mradi wa huo unaolenga kuimarisha miundombinu ya shule za awali na msingi
" Mradi huo unategemewa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitano na mwaka huu wa kwanza ndio tumepokea fedha hizo na utekelezaji wa mradi huu wa madarasa ni kwa miezi mitatu .amesema Hussen.
Amesema kupitia mradi huu wa BOOST katika awamu ya kwanza watajenga madarasa 22 na matundu ya Vyoo 15 na matawanyiko wake ni Shule ya Msingi Narumu madarasa matatu, Kengereka madarasa manne, Kawaya kati madarasa manne, Kikavu chini madarasa manne, Mkalama madarasa manne, Msamadi darasa 1 la watoto wenye mahitaji maalum na matundu 3 ya vyoo pamoja na shule mpya katika eneo la Mlima Shabaha.
Kwaupande wake Afisa Elimu Takwimu Wilayani Hapo Jafari Zaid ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo amesema ujenzi huo wa madarasa utafanyika kwa uadilifu na uamkini na utamalizika kwa muda uliokusudiwa .
Kwaupande wake Afisa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU Wilayani hapo Amani Fransis amezitaka Kamati zitakazoenda kusimamia miradi hiyo ya ujenzi kuisimamia miradi hiyo vyema huku ikiwashirikisha wananchi juu ya ujenzi huo kwani kamati ndio kila kitu katika masuala ya usimamizi wa ujenzi kwani kamati ikivurugana Miradi haiwezi kwenda vizuri
Amesema endapo litatokea suala lolote lenye viashiria vya rushwa watoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai