Ofisi ya Waziri Mkuu imeipongeza wilaya ya Hai kwa kuwa na mpango mathubuti wa kukabiliana na maafa ikiwa ni pamoja na kuwa na mkakati wa kupunguza vihatarishi vya maafa.
Pongezi hizo zilitolewa na Prudence Con- stantine ambae ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya uratibu wa maafa, ofisi ya waziri Mkuu katika kikao mkakati cha kujiandaa na kukabiliana na maafa kilichofanyika katika ukumbi wa hamashauri hiyo.
“niwapongeze wilaya ya Hai kwa kutambua umuhimu wa kuwa na mpango wa kujiandaa kukabiliana na maafa na nitumie nafasi hii kutoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ,Mkurugeni Mtendaji na Katibu Tawala wa wilaya kwa- kusimamia vema hatua zote za mpango huu” alisema Alisema kuwa ongezeko la
matukio ya majanga ambayo yamekuwa ya- kisababisha maafa na kuathiri mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii na kupelekea madhara mbali mbali kama vifo, ulemavu wa kudumu, uharibifu na upotevu wa ma- li ,ongezeko la tegemezi kutokana na watoto kupoteza wazazi.
Awali akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Hai, Afisa Tawala wilaya ya hiyo Mary Mnyawi alizitaka divisheni na vitengo na taasisi mbali mbali kuzingatia mkakati huo katika kutekeleza vipaumbele vya kisekata.Mnyawi pia aliagiza mpango huo kuwafikia viongozi wa vijiji na vitongoji na wananchi kwa ujumla ili kunapotokea maafa kila mmoja awajibike kulingana na nafasi yake.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai