Zaidi ya kesi zipatazo 84 za mirathi zimeshughulikiwa kwa kutolewa ufumbuzi huku vyombo vya usimamizi wa mabaraza ya kata yanayohusika na kesi za mirathi pamoja na ardhi kuvunjwa kwa kusindwa kutekeleza wajibu wake wa kutatua migogogro inayowasilishwa kwao.
Akizungumza kuhusu uwepo wa mabaraza butu ya kata; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewata wananchi kujiandaa kwa kuacha wosia wenye lengo la kuondoa changamoto zitakazojitokeza ikiwemo ugomvi wa kifamilia na kudhulumiwa haki haswa watoto.
“Natoa rai kwa wananchi wote katika Wilaya ya Hai kuwa na tabia ya kufanya maandalizi kwa kuandaa wosia ambao utachanganua mgawanyo wa mali ili kuepuka kutokea migogoro mtu anapofariki” Amesema Sintoo.
Ameongeza pia uwepo wa uelewa mdogo wa wananchi kuhusu sheria za mirathi na kuzitaka taasisi za kiserikali na mashirika binafsi yanayoshughulikia haki za binadamu kuelimisha jamii kuhusu swala la mirathi ili kupunguza matukio ya ugomvi ndani ya jamii.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Hai Upendo Wela amewashukuru wataalamu walioshiriki kwenye zoezi hilo huku akibainisha uzito wa zoezi hilo la kuwasaidia wananchi kupata haki zao na zaidi kuwaelimisha kuhusu masuala ya mirathi na umuhimu wa kuandika wosia.
“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imekuwa ikipokea mashauri ya mirathi na kuyashughulikia lakini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria, wakuu wa idara na taaasisi nyingine tumeweza kushughulikia mashauri mengi zaidi” Amesema Wella.
Pia wakili mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa swala la mirathi na kesi za ardhi zimekuwa kubwa kwa wilaya ya Hai huku pakiwa na uwelewa mdogo wa uandikaji wa wosia na mirathi kinachopelekea baadhi ya watu kupora mali za wengine kwa kutumia uwezo wa kifedha au nafasi za madaraka na mamlaka walizonazo.
Kwa namna nyingine mmoja wa wahanga wa kesi ya mirathi Bi Mariamu ameishukuru serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya kwa kuendesha zoezi hilo na kuwasaidia wananchi kupata haki zao na kubainisha kuwa kuna idadi kubwa ya watu wanaodhulumiwa haki zao na kushindwa kupata utatuzi wa kisheria kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuogopa kulogwa na kupoteza haki zao bila ya ufafanuzi wa sheria husika.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ametengeneza utaratibu wa kukutana na wananchi na kuwaikiliza na kuwatataulia kero wananzokutana nazo kwenye masuala mbalimbali akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya na Wataalamu wake; utamaduni ambao umepokelewa vizuri na wananchi kwa kujitokeza kupata huduma husika.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai