Katika kutekeleza agizo la kisheria la kila Halmashauri nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwaajili ya kuwawezesha wanawake, vijana na walemavu, wilaya ya Hai imetoa Zaidi ya Shilingi million 84 kwa vikundi 16 vya wanawake, vijana na walemavu ikiwa kama mkopo kwa lengo la jamii hiyo kupiga hatua katika kujikwamuwa kiuchumi na kuchochea ukuaji wa pato la taifa.
Akikabidhi hundi ya fedha hizo hii leo katika ukumbi wa maktaba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ya Hai Yohana Sintoo amesema kuwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato umechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa fedha hizo.
Amesema kuwa wanakikundi wanaopata mikopo hiyo watambue kuwa imeshatengenezewa sheria na kanuni zake hivyo Halmashauri ya wilaya ya Hai kupitia utoaji wa mikopo hiyo tayari inatekeleza sehemu yake ya sheria hiyo.
Aidha amewataka wanavikundi hao kwenda kuwekeza kwenye miradi yenye tija hasa kupitia elimu waliyopatiwa juu ya matumizi sahihi ya mikopo hiyo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella amewataka kutumia fedha hizo kwa malengo sahihi ili kuleta maedeleo kwenye jamii zao na kwa uchumi wa Taifa kama lilivyo lengo la serikali.
Nao baadhi ya wanavikundi hao wameipongeza serikali wilayani Hai kwa kuwaamini na kuwapa fedha hizo na kuahidi kwamba zitaenda kuzalisha na kwamba watarudisha kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Hai imetoa mikopo hiyo kutokana na asilimia kumi ya makusanyo ya mapato ya ndani ambapo 4% kwa ajili ya wanawake, 4% kwa vijana na 2% kwa watu wenye ulemavu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai