Wilaya ya Hai imezindua rasmi mpango wa kujiandaa kukabili maafa na Mkakati wa kupunguza vihatarishi vya maafa ikiwa ni miongoni mwa wilaya mbili pekee nchini zenya mpango huo hadi sasa.
Akizindua mpango huo mkuu wa wilaya hiyo Amiri Mkalipa amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mipango mizuri ya kuakikisha ofisi zake zinaweka utaratibu wa kukabiliana na mafaa na majanga huku akiahidi wilaya hiyo kuutumia vizuri mpango huo ulioratibiwa kwa ushirikiano na ofisi ya waziri mkuu Tanzania.
“kwanza tunayo furaha ya kupata heshima kuzindua mpango huu ni jambo la heshima wilaya ya Hai kuiteua kuwa moja katika wilaya mbili hapa nchini zinazozindua mkakati huu tunawaahidi mkakati huu tunauanzia chini kuja juu katika kuhakikisha wilaya ya Hai inakuwa ya mfano katika kukabiliana na maafa na majanga ndani ya wilaya yetu tufikishie salamu kwa mkurugenzi wa kuzuia maafa ofisi ya waziri shirika la UNCEF na Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan”
Mkalipa ameitaka kamati ya maafa ya wilaya hiyo kuchukua nyenzo husika kama sehemu ya kupunguza maafa huku akiwataka kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwa ngazi zote za vijiji, vitongoji na kata na kuwa na vikao vya mara kwa mara kuhakikisha mpango huo unafanya kazi kwa ufanisi na sio kusubiri mpaka maafa yatokee ndipo wakutane.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Edmund Rutaraka pamoja na shukrani kwa serikali kuhusu mpango huo ameahidi kuhakikisha mkakati huo utafanyiwa kazi kwa uaminifu mkubwa kwa kushirikiana na baraza la madiwani wa wilaya hiyo, mkurugenzi mtendaji na viongozi wengine kuhakikisha watu wote wa halmashauri hiyo wanaufahamu mpango huo na kuusimamia vyema kwa ajili ya utekelezaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai