KATIBU Mkuu Wizara ya Maji,Profesa Kitila Mkumbo amesitisha shughuliza za Water Service Facility Trust (WSFT), katika kutoa huduma ya maji mkoani Kilimanjaro ili kutoa fursa ya uchanguzi na kushughulikia changamoto za kisheria ikiwemo kukidhi matakwa ya sheria ya huduma ya maji na usafi wa mazingira namba 12 ya mwaka 2009.
Uamuzi wa Pro, Mkumbo unatokana na mgogoro wa mda mrefu wa uhalali wa taasisi hiyo kufanya kazi ya huduma za maji , kutokana na kutosajiliwa kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa sheria husika na kumekuwepo na ubadhilifu wa mali za umma hali iliyisababisha uongozi wa wilaya kuchukua hatua za kuzifunga ofisi za WSFT.
Kufuatia uamuzi huo , katibu huyo alisema kipindi cha mpito Wizara imeagiza mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA),kusimamia majukumu ya WSFT na kuhakikisha kuwa Bodi za watumia maji katika wilaya za Hai na Siha zinaendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Hata hivyo Prof Mkumbo alisema wakati ahatua za mda mrefu , Wizara ya Maji imeanza mchakato wa kuanzisha mamlaka ya maji katika maeneo husika ambayo itakuwa na jukumu la kutoa huduma ya maji
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo , Lengai Ole Sabaya ,alisema kuwa sepember 24 mwaka kamati ya ulinzi na usalama pamoja na uongozi wa halmashauri ulisitisha huduma zote zilizokuwa zikitolewa na WSFT baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa kufuata taarifa muhimu tatu ambazo zilitokana na kamati ya ulinzi , baraza la madiwani na taarifa ya ukaguzi
“Mheshimiwa katibu mkuu , kamati iliamua kuchukua maamuzi kutokana na uchunguzi wa kina ya namna ya kujiendesha , baraza la madiwani lilionelea kuwa kazi zinazofanywa na bodi hiyo zingeweza kufanya na bodi za maji zilizoko” alisema
“Pia imebainika kuwa katika taarifa ya mapato imekuwa haikaguliwi na wale kutoa tarifa za mapato na pili imebaika taarifa nyingine za kijinai , imebainika matumizi mabaya fedha , mali za umma zilizokuwa zinamilikiwa na mradi ambazo zilipaswa kuwa zimekabidhiwa serikalini kutokana na sababu hizo tukaamua kusitisha huduma” alisema Ole Sabaya
Kwa upande wake Mwenyekiti wa MUWSA, Pro Bee alisema kuwa maagizo yaliyotolewa na Wizara yatafanyiwa kazi na kuhakikisha kuwa wananchi wa wilaya zote zilizokuwa chini ya WSFT zinaendelea kupata huduma .
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai