Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imepokea zaidi ya shilingi Bilioni 2.4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika halmashauri hiyo.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya majengo katika halmashauri hiyo leo katika kikao cha kamati ya Ushauri ya wilaya Mhandisi wa Ujenzi wilaya John Sospiter amesema kuwa fedha hizo zimetoka serikali kuu, wadau wa maendeleo na michango ya vyama vya ushirika.
Amesema kuwa fedha hizo zimetolewa kwa kipindi cha mwaka wa 2018/2019 na 2019/2020 ambapo zitaenda kwenye ukarabati wa shule za msingi na sekondari ikiwemo ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na choo cha matundu manne katika shule ya sekondari Longoi pamoja na ujenzi wa vyumba vine vya madarasa na choo cha matundu matano katika shule ya msingi kibaoni ambapo itagharimu zaidi ya shilingi milioni 85.
Aidha ameongeza kuwa fedha hizo zinahusika katika ujenzi wa kituo cha afya Longoi kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 323, ujenzi wa vyumba saba vya madarasa, ofisi ya waalimu na choo cha walimu katika shule ya msingi kibohehe ambapo zinatumika zaidi ya shilingi milioni 206 hali itakayosaidia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule hiyo.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmasahauri ya Wilaya ya Hai kikiwakutanisha madiwani wateule wa kata 17, watendaji wa kata, maafisa tarafa na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri hiyo kikiongozwa na mwenyekiti wake Pendo Wella ambae pia ni Katibu Tawala wa wilaya akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai