Jumla ya kiasi cha shilingi 773,100,000 kimepokelewa na halmashauri ya wilaya ya Hai kwaajili ya ujenzi wa shule mpya katika kata mbili za wilaya ya Hai lengo likiwa na kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
Hayo yameelezwa na Mkuuu wa division ya elimu msingi ndugu Hussen Kitingi wakati akitambulisha miradi katika kata ya masama kusini katika wilaya ya hai.
Amesema kati ya fedha hizo sh mil.351,500,000/=ni za ujenzi wa shule ya mpya ya msingi katika kata ya masama kusini , 351,500,000 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi kata ya Machame Magharibi pamoja na shilingi 70,100,000 kwa ajili ya kujenga madarasa mawili ya mfano katika shule ya msingi Nkwanara kata ya Machame Magharibi.
Aidha amesema kuwa mrdi wa shule za boost unatakiwa kukamilika baadaya miezi mitatu ikiwa na lengo la kupunguza msongamano madarasi na kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali wa muda mrefu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha kwasadala ndugu Edmen Massawe ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kuleta fedha hizo zitakazo itakayo ondoa changamoto ya Watoto kutembea umbali mrefu.
Naye mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Doglas Neleko amesema kutokana umuhimu wa elimu uliopo kwa sasa wameupokea mradi huo wa boost awamu ya pili ambapo utasaidia kuongeza shule mpya ambazo zitasaidia watoto kujisomea na kupata haki ya elimu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai