Zaidi ya wakulima 30,000 wanatarajiwa kunufaika na ruzuku ya pembejeo inayotolewa na serikali katika msimu wa kilimo mwaka 2022/2023.
Akizuzungumza katika mahojiano maalumu mkuu wa divisheni ya kilimo, mifugo na uvuvi wilaya ya Hai, David Lekei amesema ili wakulima waweze kupata ruzuku hiyo wanapaswa kujisajili kwa mtindo wa kidigitali ambao utawezesha kutambua wakulima wote wilayani hapa ambao wanaweza kupata pembejeo za kilimo kwa bei ya punguzo la serikali.
Lekei amesema kuwa zoezi hilo la usajili linafanyika hadi tarehe 30/09/2022 na wakulima wote wanapaswa kusajili katika kipindi hicho ili kutumia vema fursa hiyo iliyotolewa na serikali.
“Niwaombeni wakulima wilayani hapa hakikisheni mnajiandikisha kwenye ofisi za watendaji wa vijiji na kata orodha itakayotoka kwenye ofisi hizo ndio itakayotumika kupata huduma za pembejeo za ruzuku”amesema Lekei
“watakaoshindwa kujisali na majina yao kukosekana kwenye orodha watakosa huduma ya ruzuku ya pembejeo”amesisitiza Lekei
Amesema kuwa serikali imeamua kutumia mfumo wa kitigitali mpango wa ruzuku ya mbolea ili kuongeza ufanisi kwa wakulima na kuwaondolea mzigo kutokana na upandaji wa pembejeo hizo.
Hadi sasa jumla ya wakulima 22,900 wilayani Hai wameshasajiliwa kwenye mfumo huo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai