Zaidi ya wananchi 55,800 wa wilaya ya Hai kata za muungano, bomang’ombe na bondeni wanatarajiwa kuondokana na tatizo kubwa la maji ambalo lilikua likikabili kata hizo kwa muda mrefu.
Hayo yamebainishwa na mwakilishi wa meneja wa Ruwasa wilaya ya Hai Daniel Benedict katika ziara ya kikazi iliyoongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka, oktoba 19 eneo la kikafu-soka ,ambapo amesema hatua zinazoendelea kwa sasa ni uchimbaji wa mitaro.
Vilevile katika taarifa yake ameongeza kuwa miongoni mwa kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mradi huo ni Ujenzi wa tenki la ujazo wa lita laki tano, ujenzi wa tenki la kukusanyia maji lita elfu hamsini ,ujenzi wa nyumba ya umeme, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba urefu wa km 27, na ukarabati wa tenki ambalo lipo karibu na hospitali ya wilaya ya Hai la mita 90.
“Kupitia mradi huu vijana 80 wameweza kupata ajira ambapo hilo ni zoezi endelevu mpaka kufikia kukamilika kwa mradi huu, ambapo mpaka sasa uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba umefikia asilimia 75%” alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amewaomba wananchi wanaohusika wa kata za bondeni, bomang’ombe, pamoja na masama kusini kuendelea kuwa wavumilivu kwani kazi bado inaendelea kwakuwa mkandrasi ameongezewa muda ili aweze kutimiza majukumu yake vizuri.
Hadi kukamilika kwa mradi huu unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.392 na utahudumia kata tatu za Hai mjini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai