Zaidi ya watoto elfu 44000 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua - Rubella na polio katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro katika zoezi lililoanza leo na linarajiwa kukamilika Oktoba 21 mwaka huu.
Mratibu wa chanjo wa wilaya ya Hai, Michael Ndowa, ameyasema hayo leo katika ufungunzi wa zoezi hilo lilofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya katika hospitali ya wilaya .
Ndowa amesema zaidi ya watoto 28,000 wenye umri kuanzia miezi tisa hadi miaka minne na miezi kumi na moja watapatiwa chanjo ya surua rubella huku watoto zaidi ya 16,000 wenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu watapatiwa chanjo ya polio.
“Maandalizi yamekamilika na zoezi limeanza rasmi leo sehemu mbalimbali za wilaya lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoto wanapata chanjo na kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na kutokupata chanjo hizo”.amesema Ndowa
Akizungumza katika ufunguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Hai Ole Sabaya amewataka watumishi wote kushirikiana na Idara ya Afya kuhamasisha wazazi na walezi wenye watoto kuhakikisha kila mtoto wenye umri unaostahili anapatiwa chanjo stahiki
“Serikali imegharamia gharama zote za chanjo hii na ndio maana inatolewa bure kwa watoto na hatuwezi kupoteza mtoto kwa kupooza kwa kukosa chanjo , hivyo ninyi wazazi na walezi miliofika hapa muhamasishe wengine wote washiriki kikamilifu katika zoezi hili”amesisitiza Mkuu wa wilaya
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai