Imeelezwa kuwa makakati wa Bodi ya Kahawa wa kugawa miche ya kahawa kwa wananchi bila ya malipo unawapa hamasa wataalam wa kilimo kusimamia yale ambayo yameelekezwa katika ilanai ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza katika kijiji cha Isuki kilichopo kata ya machame kati walaya ya Hai kwenye hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa miche ya kisasa ya zao hilo bure kwa wakulima iliyotolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Ndugu Dionis Myinga , mkuu wa idara ya kilimo, ushirika na umwagiliaji ndugu David Lekei amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali ya kufufua kilimo ya zao la kahawa.
Lekei amesema mkoa wa Kilimanjaro kuna mazao mengi lakini zao ambalo limeacha alama ni zao la kahawa, na kwamba limesababisha uchumi wa Kilimanjaro ukawa tofauti na baadhi ya mikoa mingine.
Ameongeza kuwa Kahawa inayolimwa katika maeno haya ya Hai ina ladha maalum kwa sababu ya ukanda huo kuwa na udongo wa kivolkaniki hivyo ufanya kahawa inayolimwa hapa kuwa ya tofauti na sehemu zingine.
Naye Mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe ameipongeza TCB kwa jitihada za kufufua zao hilo huku akiwataka wananchi walioacha kulima zao hilo kwa sababu mbali mbali kuendelea kulima kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro.
“msingi wa maendeleo tuliyonayo mkoa wa Kilimanjaro ni kahawa, ni kweli nakubaliana na ninyi bei imeyumba. Kwa hiyo ikiyumba na sisi tuyumbe?si tutafute majawabu tunairejeshaje barabarani?Ndio hiki tunacho anza kukitafuta.Nafurahi tumeanza kulima tena zao la kahawa.”alisema Saashisha.
Awali akizungumza Mkurugenzi maendeleao ya TCB Kajiru Kisenge amewataka wananchi kutoka kata tamaa na amewataka waliopewa miche hiyo waipande ili matokeo ya fedha za serikali zilizotumika imegharamia miche hiyo ionekane.
Kwa mujibu wa Kisenge jumla ya miche ambayo ilikuwa inahitajika kutokana na takwimu za waliojiandikisha ni miche 73,729.
“Lengo letu ilikuwa ni yale maeneo ambayo kuna umwagiliaji ili tuwahi kuwapa miche halafu hao wengine tuje tuwape mvua zinapoa anza kunyesha, ilibidi tutengeneze vitalu ambavyo vinazalisha miche ya kahawa na kama bodi tulifanikiwa kutengeneza vitalu 17.”
Bodi hiyo inaendelea na utaratibu wa kugawa miche hiyo kwa wananchi ambay itawagawanya kwa awamu tofauti tofauti hii ikiwa ni awamu wa kwanza iliyolenga wenye maeneo ya umwagiliaji wakati wengine watapata miche hiyo wakati wa mvua.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai