Wananchi wote wa Wilaya ya Hai waliojiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga Kura wanakumbushwa kuwa zimebaki siku 12 kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo watapata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano katika nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Nafasi Mchanganyiko) na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Nafasi za Wanawake).
Kupiga kura kwenye uchaguzi ni haki ya Kikatiba ya kila mwananchi wa Tanzania kwani ni sehemu ya kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo yanayohitajika kwenye jamii husika hivyo mwananchi wa Wilaya ya Hai usipoteze nafasi yako ya kuchagua kiongozi unayeamini atakuletea maendeleo.
Hudhuria mikutano ya kampeni ili kupata nafasi ya kuwasikiliza wagombea wakinadi sera za vyama vyao na namna watakavyotatua changamoto zilizopo kwenye jamii ili uweze kufanya uamuzi sahihi wa kuchagua kiongozi mwenye sera na mikakati madhubuti ya kutatua kero za wananchi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai