Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelihutubia na kuvunja Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tarehe 16/06/2020
Zaidi ya wanachi 27,000 wa kata za Weruweru, Mnadani na Masama Rundugai wanatarajia kunufaika na huduma ya afya kutoka katika kituo cha afya kinachojengwa katika kijiji cha Longoi kata ya Weruweru kinachokadiriwa kugharimu zaidi ya milioni 500 kutoka katika mapato ya ndani.
Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho uliofanyika leo katika Kijiji cha Longoi Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amesema ujenzi wa kituo hicho ni maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kwenda kwa wasaidizi wake lengo likiwa ni kuwaondolea kero wananchi maeno ambao hawana huduma hiyo tangu nchi ipate uhuru.
Amesema fedha za awali za ujenzi wa kituo hicho kiasi cha shilingi 388,552,415, kimetokana na michango ya vyama vya ushirika wilayani humu na kwamba kukamilika kwa ujenzi huu utakipa heshima ushirika ambao kwa mingi mingi sasa umekuwa ukituhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha.
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai