Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira amewataka watendaji na viongozi wilayani Hai kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii na ufanisi mkubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi wanaowatumikia.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Hai Julius Kakyama akizungumzia kupokea walimu wapya 12 wa masomo ya sayansi waliopangwa kwenye shule 10 wilayani humo. Aishukuru serikali kwa hatua hiyo na kuwaasa wazazi kuwahimiza watoto wao wasome masomo ya sayansi kusaidia kupatikana wataalamu wa kutosha nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa akizungumza na Madiwani wa wilaya hiyo akiwataka kuwatumikia wananchi kwa kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo na kuahidi kumshughulikia mtu yeyote atakayekwamisha maendeleo ya wananchi.
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai