Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya Amesitisha shughuli za uchimbaji wa Madini ya Ujenzi katika wilaya hiyo hadi hapo changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo zitakapopatiwa ufumbuzi.
Serikali imeanza kuwaandaa wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuendelea kupata tija kwenye shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kutumia mwongozo wa kilimo unaohimili mabadiliko ya tabianchi wa mwaka 2017 unaoainisha mbinu na teknolojia za kuwaongoza watunga sera na watoa maamuzi, maafisa ugani, wakulima, wafugaji na wavuvi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Capten Mstaafu George Mkuchika amebainisha mpango wa Serikali wa kuwafikia wananchi wote wenye uhitaji na kuwasaidia kuwajengea uwezo ili waweze kujimudu kiuchumi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai